Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu sita wauawa huko Beni, Kivu Kaskazini

Watu sita wauawa huko Beni, Kivu Kaskazini

Watu sita wameuawa wakati wa mapigano kati ya waasi wa ADF na jeshi la serikali FARDC huko Beni, jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Yaripotiwa kuwa majira ya mchana siku ya Jumatatu, waasi hao waliingia kituo cha afya cha Kitevya kilicho kilometa 200 kutoka upande wa doria wa jeshi la serikali, FARDC na kupora dawa zote.

Ripoti zilifikia jeshi la serikali na ndipo mapigano yalipoanza na kusababisha vifo vya raia sita, miongoni mwao wanawake wanne na wanaume wawili, huku majeruhi wakiripotiwa kuwa ni wawili.

Makundi ya kiraia huko Beni yana wasiwasi juu ya shambulio hilo kwenye eneo hilo ambako tangu mwishoni mwa wiki, jeshi la serikali na kikosi cha kujibu mashambulizi cha MONUSCO, FIB wamepiga kambi ili kukabiliana na waasi hao.