Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiwekeza kwa mtoto wa kike umewekeza kwa jamii:UNFPA

Ukiwekeza kwa mtoto wa kike umewekeza kwa jamii:UNFPA

Shirika la Umoja wa mataifa la idadi ya watu UNFPA kwa ushirikiano na serikali ya Sudan Kusini Jumatatu wamezindua ripoti ya hali ya idadi ya watu nchini humo kwa mwaka 2016.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi mwakilishi wa UNFPA Sudan Kusini

Esperance Fundira, amesema mamilioni ya wasichana wanapovunja ungo, kwao ni mwanzo wa maisha ya umasikini, kutokuwa na uwezo na kukosa fursa . Amesisitiza uwekezaji kwa wasichana wa miaka 10 kunaweza kusaidia kuleta mustakhbali bora kwa familia, jamii na taifa.

(SAUTI ESPERANCE FUNDIRA)

“Msichana anapofurahia haki zake , anaweza kusoma, kuwa na afya na kulindwa kutokana na ndoa za utotoni na mimba za mapema., na uwezo wake unaweza kufikiwa anapofikia utu uzima.”