Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili wahitajika kunasua Afrika dhidi ya madhara ya tabianchi

Ufadhili wahitajika kunasua Afrika dhidi ya madhara ya tabianchi

Dola bilioni 5.5 zinahitajika ili kukabliana na madhara ya mabadiliko ya tabainchi yanayoshuhudiwa katika nchi zilizoko kusini mwa Afrika. Hayo ni kwa mujibu wa Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya El Niño na mabadiliko ya tabianchi, Balozi Macharia Kamau.

Balozi Kamau akizungumza na idhaa hii amesema nchi kama vile Msumbiji na Botswana zinakabiliwa na hali ngumu ya ukame huku njaa ikishuhudiwa miongoni mwa watu na wanyama wakifa. Kadhalika amesema mbali na athari zinazoshuhudiwa hivi sasa kutokana na El Nino mwenedo huu unatarajiwa kuendelea katika miezi ya mwisho wa mwaka huu na mwakani kutokana na madhara ya Lanina.

Balozi Kamau ameongeza kwamba kufikia sasa Umoja wa Mataifa umepokea nusu tu ya ombi la ufadhili kwa ajili ya kukabiliana na madhara hayo na hivyo...

(Sauti ya balozi Kamau)