Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa matukio kambi ya Terrain Juba

Ban amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa matukio kambi ya Terrain Juba

Kiongozi wa tume huru maalumu ya uchunguzi kuhusu ghasia zilizotokea Juba, Sudan Kusini mwezi Julai, leo amewasilisha ripoti ya uchunguzi wa mashambulizi na visa vya ubakaji vilivyotokea ndani na karibu ya jengo la Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS na kama ujumbe huo ulitekeleza wajibu wake kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa.

Meja Jenerali mstaafu Patrick Cammaert ambaye aliyechaguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema tume yake imefanya mahojiano na watu 67, wakiwemo waathirika, serikali na mashahidi wengine kuhusu matukio mawili, moja la tarehe 8 na 25 Julai katika kituo cha kulinda raia ndani ya jengo la UNMISS na jingine katika kiwanja kiitwacho Terrain iliyo miili 1.5 karibu na jengo la UNMISS.

Amesema uchunguzi umebaini mchanganyiko wa mambo katika kutekeleza mamlaka UNMISS iliyopewa ambayo ni kulinda raia, akisema.

( SAUTI CAMMARERT)

‘‘Kwanza kabisa, tumebaini kulikuwa na ukosefu wamaandalizi ya kijeshi katika mazingira yasiyo ya kivita, na pili nchi zinazochangia polisi na jeshi kwenye Umoja wa Mataifa zilisita kutekeleza mamlaka ndani ya vituo vya usalam vya Umoja wa Mataifa.’’

-