Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya tumbaku tumia mitandao ya kijamii kwahitaji mpango wa kiamataifa:WHO

Sekta ya tumbaku tumia mitandao ya kijamii kwahitaji mpango wa kiamataifa:WHO

Matumizi ya tovuti kuchagiza uraibu kama wa sigara yametajwa kama moja ya changamoto kubwa katika juhudi za kimataifa za kupunguza uvutaji sigara wamesema wataalamu wa afya wa Umoja wa Mataifa Jumatatu.

Katika wito wa kuchukua hatua kabla ya mkutano wa kimataifa wa udhibiti wa bidhaa za tumbaku , shirika la afya duniani WHO limesema, nchi ni lazima zishirikiane kufuatilia matangazo hoyo kila pembe duniani.

Suala hilo ni moja ya masuala yatakayojadiliwa na waunga mkono mkataba wa WHO kuhusu udhibiti wa tumbaku ambao watakutana wiki ijayo mjini New Delhi. WHO inaamini kwamba sekta ya tumbaku inatafuta mianya kwenye udhibiti wa matangazo ya tovuti ili iweze kuuza bidhaa zake. Dr Vera Luiza da Costa e Silva, anatoka kwenye mkataba wa kimataifa ulioanza kutekelezwa 2005.

(SAUTI DR VERA)

"Siku hizi unaweza kuchukua filamu kutoka kwenye mtandao wa intaneti na kutazama watu wakivuta, na kuonyesha kama ni tabia ya kawaida, inabadili kabisa mazingira ya kutangazisha bidhaa za tumbaku”

Ameongeza kuwa kukuwa kwa mitandao ya kijamii kumewezesha sekta ya tumbaku kuwalenga vijana wapya.