Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna mshindi mgogoro Yemen: UM

Hakuna mshindi mgogoro Yemen: UM

Umoja wa Mataifa umewahakikishia viongozi wa kisiasa nchini Yemen , kuwa hakuna mshindi katika mgogoro unaofukuta nchini humo na kulitaka taifa hilo kukubali mpango wa mchakato wa amani.

Mchakato wa awali wa kusaka amani nchinio humo haujazaa matunda.

Akiongea wakati wa mkutano wa baraza la usalama, ulioangazia hali mashariki ya kati hususani Yemen , mwakilishi maalum wa UM nchini humo Ould Cheikh Ahmed amesema.

(SAUTI AHMED)

‘‘Baada ya miezi 18 ya mapigano ya kuogofya, maelfu ya vifo, majeruhi, madhila yasiosemekana na kuanguka kwa uchumi, tunahitaji kuhoji hadi lini Wayemen watasalia mateka wa uamuzi binafsi na wa kizembe wa kisiasa? Pande zinasubiri nini kutia saini makubaliano ya kisiasa? Mchakato niliopendekeza unaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa kwa kuwa inatoa suluhishao mujarabu.’’

Machafuko nchini humo yamesababisha vifo vya takribani watu elfu kumi na asilimia 80 ya watu nchini humo ambao ni zaidi ya milionio 20 wana uhitaji wa kibinadamu