Uchumi wa Kenya kukua kwa 6% mwaka 2017-Benki ya Dunia

31 Oktoba 2016

Uchumi wa Kenya unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka 2016 kutoka asilimia 5.6 mwaka 2015 imesema leo ripoti ya kiuchumi ya Benki Kuu ya dunia.

Kulingana na ripoti hiyo ukuaji wa uchumi wa Kenya umeendelea kuimarika katika kipindi cha miaka minane iliyopita na hali hii inatarajiwa kuendelea katika nusu ya mwaka, huku ukuaji uchumi ukitarajiwa kupita asilimia 6 mwaka 2017 na 2018.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa kuchangia ukuaji huu ni sekta bora ya kutoa huduma, ujenzi, kuongezeka kwa idadi ya watu wenye kipato cha wastani, kuongezeka kwa fedha zinazotumwa kutoka nje na uwekezaji wa umma katika sekta ya kawi na usafiri.

Akizungumzia ripoti hiyo mkurugenzi mkuu wa benki ya dunia nchini Kenya Diarietou Gaye amesema, Kenya inasalia kuwa moja ya nchi zenye kutia matumaini miongoni mwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kwani ukuaji wake wa kiuchumi umepita wastani wa kikanda wa asilimi 1.7 kwa mwaka 2016.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter