Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 5 wakabiliwa na njaa Somalia:WFP

Watu milioni 5 wakabiliwa na njaa Somalia:WFP

Zaidi ya watu milioni tano nchini Somalia hawana chakula cha kutosha, na zaidi ya milioni moja kati yao wanahitaji msaada wa kuokoa maisha, amesema mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP nchini Somalia.

WFP na washirika wake wanaongeza juhudi za kuzisaidia jamii kukabiliana na ukame mkali uliosababishwa na El Niño. Uwezo wa jamii hizo ambazo zimekumbana na misimu minne ya ukosefu wa mvua umefika kikomo.

Mkuu wa WFP Somalia Laurent Bukere anaelezea hofu yake kuhusu kupungua kwa uhakika wa chakula na nini ofisi yake inafanya kuepuka janga kubwa la kibinadamu.

(SAUTI YA BUKERE)

"Tunachokishuhudia hivi sasa ni kuongezeka zaidi kwa haki ya ukame, Kaskazini katika eneo la Puntlanda ambako mvua hazijanyesha , pia Kusini ambako ni kukame kabisa."