Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumza na Rais Zuma kuhusu ICC

Ban azungumza na Rais Zuma kuhusu ICC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma, akimshukuru kwa mchango wake katika masuala ya amani Afrika na suala la mabadiliko ya tabianchi.

Vile vile amemueleza Rais Zuma kuwa amesikitishwa sana na uamuzi wa nchi hiyo wa kujitoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu,ICC, na ameisihi nchi hiyo kuendelea na juhudi zake katika masuala ya haki na uwajibikaji, na ni matumaini yake kuwa nchi hiyo itazingatia uamuzi wake kabla haujatekelezwa miezi kumi na mbili ijayo.
Ban pia ameiomba nchi hiyo kutoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kukomesha uhasama na kurudi katika mchakato jumuishi wa kisiasa.