Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa msichana upo mikononi mwa mvulana:UNFPA

Ulinzi wa msichana upo mikononi mwa mvulana:UNFPA

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA Dkt. Natalia Kanem amesema wavulana ndio wenzi wa wasichana na hivyo sauti zao katika ulinzi wa wasichana ni muhimu.

Bi Kanem amesema hayo wakati akihudhuria mkutano wa ubia kwa ajili ya afya ya wajawazito, watoto wachanga na mtoto ulioongozwa na mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto ambaye pia ni mjane wa Rais  zamani wa Afrika Kusini Graca Machel jijini Maputo, Msumbiji.

(Sauti ya Kanem)

"Kwa kweli tunafikiri hawa ndio watu watakaoleta mabadiliko mengi katika jamii, na kuleta amani ya kweli. Kijana akielewa kwamba matendo yake yanachangia katika amani, basi hilo litakua jambo zuri sana, kwani vitu hivi vingine tunayvojadili, kama afya,elimu,maji safi na chakula havitawezekana ikiwa hakuna amani. Tunapenda sana ari ya vijana, kwani ni wabunifu, wadadisi na wako tayari kufanya maamuzi ".