Skip to main content

Shambulio la ubalozi wa Urusi Syria lalaaniwa vikali

Shambulio la ubalozi wa Urusi Syria lalaaniwa vikali

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio la bomu katika ubalozi wa Urusi lililotokea jana kwenye mji mkuu wa Syria, Damascus.

Shambulio hilo la pili limesababisha uharibifu mkubwa wa jengo la ubalozi huo, na hivyo baraza limekumbusha nchi husika kuzingatia kanuni za msingi za kutoharibu majengo ya kibalozi.
Na kwa mantiki hiyo, baraza limetoa wito kwa nchi mwenyeji kuchukua hatua madhubuti za kuyalinda majengo hayo na wafanyakazi wake, na kuzuia misukosuko ya amani yenye kudhoofisha heshima yake.