Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa ndani wazidi 15,000 Mosul, Iraq: UNICEF

Wakimbizi wa ndani wazidi 15,000 Mosul, Iraq: UNICEF

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF iliyotolewa leo Ijumaa, idadi ya watu wanaokimbia makazi yao kaskazini mwa Iraq ni zaidi ya 15,000 katika siku kumi za operesheni ya jeshi la usalama la Iraq kuchukua mji wa Mosul. Wengi wanakimbilia vijiji vingine kwa jamii ambazo pia wanajikuta mashakani mashaka.

UNICEF na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa likiwemo la mpango wa chakula WFP na la wahamiaji IOM, walishiriki kwa mara ya kwanza wiki hii katika utoaji wa misaada na vifaa mbalimbali vya dharura hasa maji, vifaa vya usafi, chakula, mablanketi, vipasha joto, mataulo na timu za chanjo na wameweza kufikia kwenye vijiji vidogo ambako waliwakuta watoto na jamii zilizokimbia makwao wakiwa na upungufu wa maji safi na vifaa muhimu vya matumizi.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Iraq, Peter Hawkins amesema kuna wasi wasi juu ya hali ya watoto wanaokaa katika vijiji hivyo na kwamba wanatafuta njia madhubuti za kufikisha maji safi, kutengeneza mazingira yao na upatikanaji wa huduma za afya na chakula.

Bwana Hawkins ameongezea kuwa kuna changamoto nyingi kuweza kufikia jamii hizi, na inawabidi kupitia kando ya barabara ili kuepuka na mabomu yaliyotegwa na vikundi vya kigaidi. Kwa sasa UNICEF ina uwezo wa kusaidia watu zaidi ya 200,000 kuwapa maji safi, na kutoa chanjo kwa watoto