Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa na uwezeshaji vijana nchini Tanzania

Umoja wa Mataifa na uwezeshaji vijana nchini Tanzania

Oktoba 24 ni siku ya Umoja wa Mataifa ambapo chombo hicho chenye nchi wanachama 193 huangazia shughuli zake zinazojikita katika misingi mikuu ya maendeleo, Amani na usalama na haki za binadamu. Kuelekea siku hiyo, Umoja wa Mataifa huandaa shughuli mbali mbali ikiwemo wiki ya vijana, ambayo lengo kuu ni kuchagiza vijana hasa wakati huu ambapo ushiriki wao ni muhimu ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Tanzania ni moja ya nchi wanachama ambako Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo kwa kushirikiana na serikali iliandaa wiki ya vijana huko mkoani Simiyu. Kupitia wiki hiyo vijana walipata fursa ya kuonyesha shughuli mbali mbali ikiwemo za maendeleo.