Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eritrea ifikishwe ICC kwa ukiukaji wa haki za binadamu

Eritrea ifikishwe ICC kwa ukiukaji wa haki za binadamu

Wito umetolewa kwa jumuiya ya kimataifa kukumbuka kilio cha walioathirika wa ukiukwaji wa haki za binadamu na kutowajikika nchini Eritrea. Rosemary Musumba na taarifa kamili

(TAARIFA YA ROSE)

Wito huo umetolewa na Bi Sheila Keetharuth aliye kuwa kwenye ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi wa haki za binadamu nchini Eritrea. akiwasilisha ripoti yake kwenyebaraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Ijumaa amependekeza pia Eritrea kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC kwa vitendo hivyo na ukwepaji sheria.

Bi Keetharuth, amesema utafiti ulioipat umeonyesha wazi kesi za uhalifu tangu mwaka 1991 zilizofanywa na viongozi wa Eritrea ikiwemo utumwa, kufungwa jela, watu kupotea, mateso na vitendo vingine vya kinyama, kama ubakaji na mauaji dhidi ya raia ili kuendeleza utawala na uongozi uliopo nchini humo.