Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna wa UNHCR azuru kambi ya wakimbizi Burundi

Kamishna wa UNHCR azuru kambi ya wakimbizi Burundi

Msaidizi wa Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Volker Turk, amehitimisha ziara yake ya siku mbili hii leo. Pamoja na kukutana na viongozi wa UNHCR na maafisa wa serikali, afisa huyo amepata fursa ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya muda mkoani Cibitoke kaskazini magharibi mwa Burundi.

Kutoka Burundi Ramadhani Kibuga ana taarifa kamili.

( TAARIFA YA KIBUGA)

Hapa ni kwenye kambi ya Muda ya Cishemere , mkoani Cibitoke sio mbali sana na mpaka kati ya Burundi na JKC. Sehemu hii ndio hupitia kwa muda wakimbizi kutoka Congo kabla ya kupelekwa kwenye kamb i mbalimbali nchini kati.

Kituo hiki sehemu kubwa kuna kinamama na watoto wanaokimbia machafuko mashariki mwa Congo

Huduma ya kwanza inatolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu. Mama huyu ndio tu amevuka mpaka

Msaidi wa Kamishana wa Shirika la wakimbizi Duniani Volker Turk ameshuhudia binafsi namna wakimbizi hao wanavopokelewa na kuridhishwa saana

(Sauti ya Volker)

"Nimeguswa na nilichoona hapa, nimefurahishwa na namna yanavofanyika mahojiano maanake hamna muda mrefu kati ya kuhojiwa na maamuzi. Huu ni utaratibu mzuri , nimeupenda saana. Nimependa hakika huu ushirikiano kati ya serikali, na mashirika ya Umoja wa mataifa pamoja na shirika la msalaba mwekundu hasa namna wanavoshughulikia watu wenye shida sana kama vile wanawake na watoto ''

Mbali na kutembelea kambi hiyo ya muda ya wakimbizi , afisa huyo wa Tawi la Umoja wa Mataifa la wakimbizi amekuwa na mazungumzo na Wakuu wa Burundi akiwemo Makamu wa kwanza wa Rais Gaston Sindimwo ambae amelitaka Shirika la HCR kusaidia katika mpango wa kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Bdi waliochukua hifadhi katika jirani . Hata hivo waziri wa Burundi wa mambo ya ndani Pascal Barandagiye ameilaumu Rwanda kwa kuwazuwia makusudi wakimbizi wa Burundi kurejea nchini na kulitaka shirika la HCR kuingia kati.

(Sauti ya Waziri Barandagiye)

"Kwa wakimbizi wetu walioko Rwanda kuna Shida, Rwanda inawazuia wakimbizi kurejea kwa hiari.Anayefaulu kuja anakuja kwa kutoroka. Na anayekamatwa anakiona cha mtemakuni. Kwa hiyo tunaomba HCR kuishinikiza Rwanda kuwaacha wakimbizi kurejea kwa hiari"