Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu za rushwa Afrika zibadilike: Ripoti

Takwimu za rushwa Afrika zibadilike: Ripoti

Takwimu kuhusu rushwa barani Africa zinatumia vipimo vya mitazamo na hisia za watu, na siyo imara, amesema Eunice Ajambo, mtalaam wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika, ECA, wakati wa uzinduzi wa ripoti kuhusu utawala barani Afrika, mjini Kigali, Rwanda.

Amesema ni muhimu kutambua kiasi cha kimataifa kinachochangia katika ufisadi barani humo, hasa kupitia mitiririko ya fedha haramu.

( SAUTI AJAMBO)

"Ili kupambana na rushwa, Afrika inahitaji tasisi na sera za utawala bora ambazo haziangalii tu makosa yanoyofanyika ndani kwa sababu siyo waafrika tu ambao wanatenda rushwa barani humo." 

Bi Ajambo amesisitiza kwamba ni muhimu kugundua vigezo vya kupima rushwa venye ukweli zaidi, kwani

"Ni muhimu sana kubadilisha takwimu zetu kuhusu rushwa ambazo hazitoi picha sahihi kuhusu nchi, kwa sababu mara nyingi wawekezaji na wafadhili wanaangalia takwimu hizo kabla ya kuchukua uamuzi kuhusu kuwekeza pesa au kutoa msaada kwenye nchi fulani."