Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko Kenya kubadili hukumu za kifo kuwa kifungo cha maisha: UM

Heko Kenya kubadili hukumu za kifo kuwa kifungo cha maisha: UM

Uamuzi wa Rais Uhuru Kenyanta wa Kenya kubadili hukumu zote za kifo kuwa vifungo vya maisha jela wiki hii umekaribishwa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Uamuzi huo umewatoa wafungwa 2747 kwenye orodha ya kifo , wakiwemo wanaume 2655 na wanawake 92.

Mkataba wa kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa uliridhiwa na Kenya mwaka 1972, na unasema mtu yeyote aliyehukumiwa kifo ana haki ya kutafuta msamaha au kubadilishiwa hukumu kuwa kifungo cha maisha. Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTI YA RAVINA)

“Tunatumai kwamba hatua ya Kenya itachagiza mataifa mengine kuendeleza juhudi zao za kufuta hukumu ya kifo na kuungana na nchi 106 ambazo tayari zimeachana na hatua hiyo ya kinyama.”

Ameongeza kuwa wanatuamai huo utakuwa mwanzo wa Kenya kuifuta kabisa hukumu hiyo.