Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania kunufaika na ushirikiano wa kikanda: Balozi Ali Siwa

Tanzania kunufaika na ushirikiano wa kikanda: Balozi Ali Siwa

Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ni lazima itegemee ushirikiano baina ya nchi wanachama wake wala si mashindano, wamesema washiriki wa mjadala wa kisiasa uliofanyika wiki hii mjini Kigali nchini Rwanda kuhusu ukhirikiano wa kikanda.

Kwa mujibu wa Kaimu mkuu wa ofisi ya Afrika Mashariki ya Kamisheni ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika, ECA, Andrew Mold, chumi zote za nchi za Afrika Mashariki zimenufaika na muungano wa kibiashara wa EAC, hasa Tanzania, ambapo takwimu zinaonyesha kwamba biashara yake ndani ya EAC imeongezeka mara tatu tangu mwaka 2011.

Kwa upande wake, mwalimu Tobias Knedlik, kutoka chuo kikuu cha Bremen nchini Ujerumani amesema mfano wa Muungano wa Ulaya unapaswa kuwa somo kwa ECA, kwani unonyesha kwamba muungano wa kifedha umesababisha ushirikiano wa kiuchumi kuimarika zaidi.

Akihojiwa na Priscilla Lecomte wa Umoja wa mataifa kando ya mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ali Idi Siwa, ameanza kwa kueleza alichojifunza kupitia mjadala hayo kuhusu ushirikiano wa kikanda barani Afrika.

(MAHOJIANO NA BALOZI SIWA)