Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama wa chakula nchini Sierra Leone ni tete baada ya Ebola : Ripoti

Usalama wa chakula nchini Sierra Leone ni tete baada ya Ebola : Ripoti

Zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini Sierra Leone ikiwa ni watu milioni 3.5 wana uhaba wa chakula, na hawana uhakika wa chakula. Kati yao watu zaidi ya 600,000 hawana chakula bora. Ripoti inasema pia hawawezi kukabiliana na majanga mpya kama vile ukame, mafuriko, pia kupanda na kushuka kwa bei za vyakula, hili likiwa ni ongezeko la asilimia 60 tangu mwaka 2010.

Katika hotuba yake kwenye sherehe ya uzinduzi wa ripoti siku ya Alhamisi, Waziri wa Kilimo, Elimu ya Misitu na Chakula, Profesa Monty Jones, amesema serikali iko tayari kuunga mkono juhudi za kubadilisha sekta ya kilimo kuwa injini ya kukuza uchumi na jamii. Wengine waliohudhuria ni wawakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP na shirika la chakula na kilimo FAO.

Ripoti hiyo ni kilele cha tathmini kubwa iliyofanywa kwa kaya zaidi ya 34,000 na maeneo 149 katika wodi 18 za mijini na kuangalia uhakika wa chakula nchini. Ripoti inasema ingawa mlipuko wa Ebola ulizidisha tatizo la chakula lakini uhaba wa chakula ni tatizo sugu linayosababishwa na miundombinu inayoathiri mfumo wa uzalishaji.

Mwakilishi wa FAO nchini Nyabenyi Tipo amesema ripoti hiyo inaelezea kuwa ni asilimia 4 tu ya wazalishaji wa mpungua ndio waliowaliweza kujitosheleza na ukuzaji wa mpunga ikiwa ni punguzo la asilimia 15 kwa miaka mitano iliyopita.

Naye mkurugenzi wa WFP nchini humo amesema kupitishwa kwa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs), na takwimu sahihi za msingi zinaipa serikali na wadau wa maendeleo ili kipimo cha hatua katika kukomesha njaa ili kufikia SDG nambari 2.