Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msumbiji ijipange kukabiliana ukame mwingine- Macharia

Msumbiji ijipange kukabiliana ukame mwingine- Macharia

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya El Niño na mabadiliko ya tabianchi, Balozi Macharia Kamau, amesema athari za mabadiliko ya tabianchi zinaonekana dhahiri nchini Msumbiji ambapo kati ya watu milioni 1.5 na milioni 2.3 wanateseka na ukame ulioletwa na El Niño.

Balozi Kamau ambaye yuko ziarani kwenye ukanda wa Kusini mwa Afrika, amesema matumaini yake ni kujionea mwenyewe hali ilivyo, kuongea na viongozi kudhihirisha mshikamano wa jumuiya ya kimataifa na vile vile kuongeza uelewa wa changamoto zinazoikumba Msumbiji.

Wakati wa ziara hiyo nchini Msumbiji, Balozi Macharia amekuwa na mazungumzo na Rais Filipe Nyusi ambapo walichokubaliana ni...

(Sauti ya Macharia)

Amesema janga hilo si geni Msumbiji, lakini dhoruba yake inazidi kuwa kubwa zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi na kuisihi nchi hiyo kuondokana na utegemezi wa nje, kwa kuweka mikakati endelevu.