Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni ngumu kuondoa majonzi nikumbukapo wafanyakazi wa UM waliofariki kazini: Ban

Ni ngumu kuondoa majonzi nikumbukapo wafanyakazi wa UM waliofariki kazini: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza katika kumbukumbu ya wafanyakazi wa umoja huo waliofariki wakati wakihudumu maeneo mbalimbali zilimo ofisi za Umoja wa Mataifa.

Kumbukumbu ya leo hapa makao makuu ni ya kutoa heshima kwa wafanyakazi 210 waliofariki katika kipindi cha kuanzia Januari mosi 2015 hadi Juni 30 mwaka huu.

Katika hotuba yake Ban amesema anapata tabu kuondoa hisia za majonzi za wafanyakazi na marafiki wanaofariki wakipigania amani duniani, na kwamba licha ya kuwa Katibu Mkuu kwa takribani muongo mmoja kila inapofika kumbukumbu hiyo hupata wakati mgumu.

Amesema watu wanaokumbukwa hii leo wanatoka sehemu mbalimbali duniani, lakini kinachowaunganisha ni bendera ya bluu ya Umoja wa Mataifa ambayo ni kielelezo cha amani na hivyo.

( SAUTI BAN)

‘‘Inawakilisha dhamira kwamba kwa kufanya kazi pamoja twaweza kumfundisha mtoto, twaweza kulisha familia, twaweza kuponya jamii, twaweza kusongesha nchi na dunia yetu sehemu bora zaidi.’’