Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunapaza sauti ya mwanamke asiyesikilizwa Sudan Kusini-Bineta

Tunapaza sauti ya mwanamke asiyesikilizwa Sudan Kusini-Bineta

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika kuhusu masuala ya wanawake, amani na usalama, Bineta Diop amesema wanawake wa Sudan Kusini wamechoka kudhalilishwa na kunyanyapaliwa na wakati umewadia kuwajumuisha katika mchakato wa amani. Rosemary Musumba na Ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

Bi Diop amesema hayo akihojiwa na Radio Miraya akisema kuwa wanawake wa Sudan Kusini wametaka kuanzishwa kwa kampeni #WomenofSouthSudan, kampeni yenye maudhui ya kurejesha hadhi ya mwanamke wa Sudan Kusini.

Amesema ni vigumu kwa wanawake kusikika katika vita, na hivyo ofisi yake inachukua hatua madhubuti katika kuwalinda na kuwatetea wanawake wa nchi hiyo ambao wanateseka na ubakaji uliokithiri.

Ametoa wito kwa seriakali ya Sudan Kusini kusitisha ubakaji na kuwaleta wanawake katika meza ya mazungumzo ya amani, akisema ..

(Sauti ya Bineta)

"Katika pembe zote za Afrika na katika awamu ya maendeleo Afrika, wanawake wawe watendaji muhimu, hatutaki kuona wakiendelea kuwa waathirika bali waleta mabadiliko. Na wasiogope, bali wapaze sauti kubwa na kusema hatutaki hili tena."