Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapinduzi ya takwimu yatasaidia kuwa na dunia isiyo na njaa:FAO

Mapinduzi ya takwimu yatasaidia kuwa na dunia isiyo na njaa:FAO

Nchi na mashirika ya kimataifa yanahitaji kufanya juhudi kubwa kuongeza uwekezaji wa kuboresha uwezo wa takwimu wa kitaifa ili kufuatilia maendeleo ya kufikia ajenda ya mwaka 2030. Ujumbe huo umewasilishwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO José Graziano da Silva, wakati wa kuanza mkutano wa 7 wa kimataifa wa takwimu za kilimo kwa ajili ya kotokomeza njaa. Mkutano huo ulioandaliwa na taasisi ya takwimu ya Italia na FAO , unafanyika mjini Roma kuanzia leo Oktoba 26 hadi oktoba 28.

Bwana Da Silva amesema mahitaji ya takwimu ya malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s yanapita uwezo wa sasa wa mifumo ya nchi nyingi ya takwimu, na ili kukabiliana na changamoto hiyo dunia inahitaji kuimarisha mifumo ya ukusanyaji takwimu, kuchukua mitazamo bunifu na njia zisizo na gharama kubwa kama vile matumizi ya teknolojia ya simu au picha zinazohisiwa kwa mbali.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni uboreshaji wa takwimu za kilimo katika kusaidia agenda ya maendeleo endelevu.