Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wabunge wanawake bado changamoto-IPU

Ukatili dhidi ya wabunge wanawake bado changamoto-IPU

Ripoti mpya ya muungano wa mabunge duniani IPU inaonyesha kwamba ukatili ukiwemo wa kingono dhidi ya wabunge wanawake ni tatizo ambalo linazorotesha usawa wa kijinsia na kukwamisha misingi ya demokrasia.

Ripoti hiyo imezinduliwa wakati mkutano wa IPU ukiendelea mjini Geneva, Uswisi.

Utafiti huo uliohusisha wabunge wanawake 55 kutoka nchi 39 kwenye kanda tano za dunia umeonyesha viwango vya kusikitisha vya ukatili wa kisaikolojia, kingono na kimwili ambako wabunge wanawake wamesema hupitia ukandamizaji na ubaguzi kila siku katika kazi zao.

IPU kupitia katibu Mkuu wake Martin Chungong imetoa wito kwa mabunge kuweka sera thabiti ili kukabiliana na hali hiyo, akiongeza kwamba ustawi wa mabunge unategemea uongozi wa mfano.