Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika Kusini itafakari upya uamuzi wake-Ban

Afrika Kusini itafakari upya uamuzi wake-Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasihi Afrika ya Kusini kufikiria upya mpango wao wa kujitenga na mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC.

Katika taarifa yake, Bwana Ban amesema Afrika Kusini imechangia pakubwa katika kuanzishwa kwa taasisi hiyo, na anaamini kwamba ICC bado ni sehemu muhimu katika jitihada za kimataifa za kukomesha ukwepaji sheria na migogoro.

Nchi hiyo ilitangaza kujitoa kwenye mkataba wa Roma wiki iliyopita kufuatia tangazo la Burundi la kujitoa katika mkataba huo.