Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufumbuzi wa nishati mbadala kusaidia upatikanaji wa nishati : ESCAP

Ufumbuzi wa nishati mbadala kusaidia upatikanaji wa nishati : ESCAP

Jitihada za ufumbuzi wa nishati mbadala katika kanda ya Asia-Pasifiki unaweza kusaidia changamoto za upatikanaji wa nishati inayozikabili nchi katika kanda ya Asia-Pasiki amesema mkuu wa Tume ya Uchumi na Jamii ya kanda hiyo ya Umoja wa Mataifa (ESCAP) hii leo huko Singapore katika juma la kuadhimisha wiki ya nishati ya kimataifa.

Dkt Shamshad Akhtar ambaye ni katibu mkuu na mtendaji wa ESCAP akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa uzinduzi wa nishati ulioandaliwa na ESCAP na mamlaka ya Singapore amesisitiza kuwa maendeleo ya teknolojia na ufumbuzi wa masoko bunifu ya kifedha yanaweza kurejesha a mafanikio ya upatikanaji wa nishati kwa kizazi cha sasa.

Ametaja pia mfano wa matumizi wa teknolojia kama vile nishati ya jua, mifumo mseto, biogas na umeme wa maji ni muhimu katika maendeleo.

Dk Akhtar amesema japokuwa kumekuwa na maendeleo na ongezeka kwa upatikanaji wa nishati katika miaka ya hivi karibuni, karibu nusu bilioni ya watu katika Asia na Pasifiki bado wanakosa huduma ya umeme, ikiwemo milioni 350 kati yao katika Asia ya Kusini.