Wanawake Burundi na fursa za kuzalisha
Ulimwengu huadhimisha tarehe 15 Oktoba siku ya kimataifa ya Mwanamke wa kijijini. mwaka huu , siku hiyo imeangazia nafasi ya malengo ya maendeleo endelevu katika kuwawezesha wanawake wa mashinani na kuwajumuisha katika kuongeza maradufu uzalishaji wa kilimo na kipato cha wazalishaji wadogo wadogo.
Huko Burundi, wanawake wa Vijijini wamekuwa wanachangamkia kilimo kwa kujumuika kwenye mashirika, hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao.
Mwandishi wetu wa maziwa makuu, Ramadhani Kibuga ametembelea katika mkoani Cibitoke eneo la Rugombo lililoko kwenye mpaka wa Burundi na Rwanda na kushuhudia kasi ya kilimo cha kinamama vijijini kwenye eneo hilo. Ungana nao.