Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanaokufa maji wakisaka hifadhi yaongezeka: UNHCR

Idadi ya wanaokufa maji wakisaka hifadhi yaongezeka: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya kuwa mwaka 2016 umefurutu ada kwa vifo kwenye bahari ya Mediterranean, hadi sasa watu zaidi ya 700 wamepoteza maisha.

Idadi hiyo huenda ikawa kubwa zaidi kwani mwaka huu haujakamilika na ikilinganishwa na ile ya mwaka jana ambapo ilikuwa ni hiyo hiyo hadi mwisho wa mwaka.

UNHCR inasema katika taarifa yake kuwa mwaka jana zaidi ya watu laki moja walivuka baharini, wakati mwaka huu hadi sasa zaidi ya laki tatu wamevuka Mediterranean.

Takwimu za shirika hilo kadhalika zineonyesha kuwa mwaka jana vifo vilirikodiwa kwa wastani wa mtu mmoja kati ya 269 ilihali mwaka huu wastani ni mtu mmoja kati ya 88 na hali ni mbaya zaidi kwa safari kati ya Libya hadi Italia kwa wastani wa kifo cha mtu mmoja kati ya 47.