Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM Pakistan walaani vikali shambulio dhidi ya polisi

UM Pakistan walaani vikali shambulio dhidi ya polisi

Familia ya Umoja wa Mataifa nchini Pakistan imelaani vikali shambulio lililotokea leo dhidi ya kituo cha mafunzo ya polisi mjini Quetta.

Shambulio hilo limewalenga wanafuzi, wakufunzi na polisi wa usalama. Angela Kearney mratibu wa masuala ya kibinadamu na mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Pakistan amesema wameshtushwa sana na shambulio hilo la kikatili lililotokea leo Jumanne ambapo watu zaidi ya 60 wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.

Kwa niaba ya Umoja wa Mataifa ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga, na serikali ya Pakistan.