Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tegla Loroupe ang’ara tuzo ya UM

Tegla Loroupe ang’ara tuzo ya UM

Tegla Louroupe kutoka Kenya ameshinda tuzo ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa inayotambua mchango wa mtu binafsi katika kusongesha misingi ya umoja huo.

Bi. Louroupe ambaye ni maarufu kwa mbio za marathon, na balozi mwema wa amani wa Umoja wa mataifa, katika mahojiano na idhaa hii amesema amepokea tuzo hiyo kwa heshima kubwa,  kwani ni ishara ya utambuzi wa kazi anayoifanya hususani ikilenga wakimbizi

(Sauti ya Tegla-1)

Ameongeza kwamba kando na kuwasaidia wanawake katika  biashara pia anawalenga watoto wa jamii za wafugaji, hata hivyo bado anatilia mkazo michezo..

(Sauti ya Tegla-2)