Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wasimame kidete kutatua mizozo- Rita

Wanawake wasimame kidete kutatua mizozo- Rita

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo linakutana kuangazia azimio lake nambari 1325 la mwaka 2000 ambalo linasisitiza ushiriki wa wanawake kwenye kuzuia na kusuluhisha majanga. Brian Lehander na ripoti kamili.

(Taarifa ya Brian)

Mkutano unahutubiwa na viongozi mbali mbali akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ikiwa ni miaka 16 tangu kupitishwa kwa azimio,  huku ujumuishaji wanawake kwenye kutatua mizozo ukiwa na walakini.

Rita Martin Lopidia mwanaharakati kutoka Sudan Kusini ambaye pia anahutubia Baraza la Usalama, amesema ameshuhudia vile ambavyo mikataba ya amani isiyoweka bayana ushiriki wa wanawake isivyokuwa na mashiko, akitolea mfano huko Sudan Kusini.

Amesema licha ya sitisho la mapigano, vita iliibuka Julai, watetezi wa haki nao wakakimbia….

 (Sauti ya Rita)

“Iwapo wanawake hawatasimama kidete na kujaribu kushughulikia suala hili la mizozo, basi janga litabisha hodi milangoni mwetu, na hilo ndilo lililotokea.”