Hotuba za chuki na vitisho vyatia hofu Sudan Kusini: Zeid

25 Oktoba 2016

Hotuba za chuki na kuchochea ghasia zinazoongezeka dhidi ya makundi ya kikabila Sudan Kusini katika wiki za karibuni zinamtia hofu Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Zeid Raad Al Hussein amesema barua zilizo na onyo la kuzusha machafuko dhidi ya watu wa Equatoria, zimeacha nje ya ofisi mbalimbali za mashirika ya kibinadamu kwenye mki wa Aweil West , Kaskazini mwa Bahr el Ghazal, eneo la Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Makundi ya vijana wa kabila la Dinka wanawaonya watu wa kabila la Equatoria kwamba watawatokomeza, baada ya taarifa za kuuawa watu kadhaa wa kabila la Dinka waliokuwa wakisafiri kwa basi kuelekea Juba Oktoba 8. Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Ravina Shamdasani anafafanua zaidi

(SAUTI YA RAVINA)

“Ujumbe wa wito wa kulipiza kisasi ulisambazwa kupitia mtandao wa kijamii na kuibua hofu miongoni mwa jamii ya kabila la Equatoria kuhusu mauji ya kulipiza kisasi. Kamishna mkuu ameonya kwamba hali hiyo inazua chuki kati ya makabila ya  waDinka na waEquatoria na huenda ikasababisha janga kubwa iwapo haitakomeshwa. Ukatili dhidi ya raia unapaswa kufanyiwa utafiti na wahusika kuwajibishwa kwa ukatili wao.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter