Wahamisheni wakazi wa pori la Calais-UNHCR

Wahamisheni wakazi wa pori la Calais-UNHCR

Kambi isiyo rasmi ya wakimbizi na wahamiaji ya Calais almaarufu kama “pori” mazingira yake si salama kwa makazi ya binadamu.

Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo kwa muda mrefu limekuwa likipendekeza kufungwa kwa kambi hiyo na kuwekwa kambi rasmi kwa ajili ya waomba hifadhi na wahamiaji.

Hatimaye Jumatatu serikali ya Ufaransa imewahamisha kwa hiyari watu 1900 kutoka kwenye pori hilo na kuwapeleka kwenye vituo vya malazi sehemu mbalimbali nchini Ufaransa. William Spindler ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA SPINDLER)

''Hakuna matukio mabaya yameripotiwa, na UNHCR imekuwa hapo muda wote, ikitoa taarifa za haki za kisheria na kusaidia kutambua watu wenye mahitaji maalum wakiwamo mamia ya watoto walioko peke yao. UNHCR imetaka mpangilio maalum uandaliwe kuhakikisha usalama na ustawi wa watoto hao na hili litokee kabla kambi haijafungwa.''