Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa ndani wafungasha virago mara ya pili Gaalkacyo:OCHA

Wakimbizi wa ndani wafungasha virago mara ya pili Gaalkacyo:OCHA

Hebu fikiria baada ya kukimbia vita na kuwa mkimbizi wa ndani sasa walazimika kufungasha virago tena. Hali hiyo imewasibu aelfu ya wakimbizi wa ndani na wakazi wa mji wa Gaalikacyo katikati mwa Somalia wanaolazimika kunusuru maisha yao kufuatia machafuko yaliyozuka hivi karibuni.

Kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA watu kutoka jimbo la Galmadug na Puntland walizua tafrani mapema mwezi huu, hadi sasa watu takribani 20 wamepoteza maisha na maelfu kuzihama nyumba zao.

Ili kufahamu kinachoendelea hivi sasa Flora Nducha wa idhaa ya Kiswahili amezungumza na Tomas Nyambane afisa wa OCHA Gaalikacyo. Anaanza kwa kueleza kuanza kwa kizaazaa hicho.

(MAHOJIANO SOMALIA)