Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanunua mafuta ya elfu 50, washindwaje mtaji wa elfu 20? - TYIC

Wanunua mafuta ya elfu 50, washindwaje mtaji wa elfu 20? - TYIC

Umoja wa Mataifa unapigia chepuo vijana kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Vijana walio katika ngazi mbalimbali za elimu wanachagizwa kutumia stadi walizo nazo ili kubadili maisha yao na kuondoa utegemezi wa kusubiri kuajiriwa. Miongoni mwao ni Jane Michael, mhitimu wa Chuo Kikuu nchini Tanzania ambaye sasa yuko kwenye kikundi cha vijana wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma, TYIC. Katika mahojiano na Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo anaelezea kile wanachofanya baada ya ufadhili kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO.