Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la UM kuboresha takwimu kuhusu wanawake na wasichana

Kongamano la UM kuboresha takwimu kuhusu wanawake na wasichana

Takwimu za kuaminika na stahiki ni muhimu kwa ajili ya utekelezaji na ufuatiliaji wa maelengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs, hususani lengo nambari 5, linalohimiza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana.

Hayo ni kwa mujibu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women. Kitengo hicho kimesisitiza kwamba takwimu sahihi zinahitajika ili kuhakikisha wanawake na wasichana wakiwemo wasiojiweza wanajumuishwa hasa kwa kuzingatia, kipato, jinsia, taifa, asili yao, uhamiaji na ulemavu miongoni mwa mambo mengine.

Kitengo hicho kimeongeza kuwa kongamano la kimataifa kuhusu takwimu na jinsia linalolofanyika nchini Finland linaangalia njia za kuboresha takwimu hizo ili kuboresha sera za jinsia na kusaidia kufikia malengo ya SDGs kwa wote.

Kongamano hilo la sita la kimataifa lililoandaliwa na idara ya Umoja wa Mataifa takwimu (UNSD), kwa kushirikiana na kitengo cha takwimu cha Finland, linafanyika mjini Helsinki kuanzia leo 24 hadi 26 Oktoba