Miaka 20 bila mbun’go Zanzibar asante IAEA

Miaka 20 bila mbun’go Zanzibar asante IAEA

Miaka 20 iliyopita msimu kama huu kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania , kilikuwa cha kwanza barani Afrika kutokomeza mbun’go, shukrani kwa teknolojia ya nyuklia.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA, Kabla ya kukomeshwa kwa mbun’go hao , ugonjwa wa nagana unaoenezwa na mbung’o ulikuwa unakatili maelfu ya mifugo na kukipa kisiwa cha Unguja hasara ya dola milioni 2 kwa mwaka.

Khalifaa Saleh kutoka wizara ya kilimo ya Zanzibar aliyesimamia kampeni na mradi wa kitaifa wa kutokomeza mbung’o, amesema kumalizika kwa wadudu hao na maradhi ya nagana kisiwani Unguja ni moja ya mafanikio muhimu sana katika kuboresha kilimo na ufugaji kwa wakulima wa Unguja katika miaka 20 iliyopita.

IAEA inasema teknolojia ya kuwafanya wasizaliane mbung’o hao imekuwa kichocheo kikubwa cha mafanikio ya kutokomeza kabisa kizazi cha mbun’go na maradhi ya nagana kutoka asilimia 19 hadi asilimia sufuri.

Kutokomezwa na nagana kumesaidia kupunguza matatizo ya kuharibika kwa mimba wa ng’ombe, vifo vya ndama na kuongeza uzalishaji wa maziwa na nyama.