Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano Gaalkacyo yakatili watu 18 na kujeruhi 60: OCHA

Mapigano Gaalkacyo yakatili watu 18 na kujeruhi 60: OCHA

Mapigano yamekuwa yakiendelea kwa wiki ya tatu mfululizo kwenye mji wa Gaalkacyo katikati mwa Somalia. Hadi sasa watu 18 wameshapoteza maisha , 60 kujeruhiwa na wengine zaidi ya elfu 75 kutawanywa , limesema shirika la kuratibui masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.

Kwa mujibu wa shirika hilo idadi inaweza kuwa kubwa zaidi kwani maelfu ya watu wanaendelea kufungasha virago. Mapigano mapya makubwa yalizuka mwishoni mwa wiki ambapo kwa Jumamosi pekee watu sita waliuawa na 21 kujeruhiwa na OCHA inasema asilimia 20 ya waathirika ni raia.

Wakimbizi wa ndani 20,000 waliokuwa kwenye makazi ya Kusini mwa Gaalkacyo sasa wamehamishwa na asilimi 60 ya wakimbizi wa ndani Kaskazini mwa mji huo wameshamishiwa kwenye makazi mengine vijijini. Juhudi za serikali ya Somalia kurejesha amani kwenye mji huo zinaendelea.