Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukosa lishe bora ni umasikini

Kukosa lishe bora ni umasikini

Katika mfululizo wa makala kuhusu dhima ya umasikini na hatua za kuukabili, leo tunamulika Uganda, ambapo tunaelezwa kuwa licha ya umasikini wa kipato, wananchi wanahitaji uwekezaji katika lishe bora itakayowaepusha na magonjwa na kadhia ngingine.

John Kibego kutoka nchini humo anazungumza na wakazi wa Hoima na wadau wa maendeleo wanaoeleza namna wanavyouelewa umasikini na namna ya kuutokomeza.