Di Caprio umefanya kazi nzuri kuhusu mabadiliko ya tabianchi- Ban

Di Caprio umefanya kazi nzuri kuhusu mabadiliko ya tabianchi- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni kweli kuwa mabadiliko ya tabia nchi yameletwa na binadamu na kusababisha madhara makubwa.Ameyasema hayo Alhamisi mjini New York baada ya kuangalia filamu iitwayo #BeforeTheFlood au kwa kiswahili “Kabla ya Mafuriko”.

Akimsifu Leonardo DiCaprio aliyecheza filamu hiyo, Ban amesema alivutiwa dhamira yake ya kuokoa mazingira ya kimataifa na akamteua kuwa mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuchagiza kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Pia alimshukuru mwongozaji wa filamu hiyo Fisher Stevens, shirika la National Geographic na wote waliohusika kwa kuonyesha filamu na hali halisiya hali ya hewa.

Katibu mkuu amesema kupitia filamu hiyo, DiCaprio ameonyesha changamoto iliyopo , lakini muhimu zaidi jinsi ya kukabiliana nayo.Amesema DiCaprio ambaye alihudhuria mkutano wa kihistoria huko Ufaransa kwenye sherehe ya kutia sainia mkataba wa Paris. Mkataba huo utaanza kutekelezwa tarehe 4 Novemba mapema kuliko ilivyotabiriwa.

Ban amesema mkataba wa Paris unaonyesha umuhimu wa sekta zote za jamii kukabiliana na changamoto ya hali ya hewa na serikali katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni Segolene Royal waziri ya Ufaransa wa mazingira na John Kerry, waziri wa mambo ya nje wa Marekani.