Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya umaskini Afrika Mashariki na mbinu za kukabiliana nao

Hali ya umaskini Afrika Mashariki na mbinu za kukabiliana nao

Umasikini, umasikini!

Nini hasa maana yake na athari zake katika maendeleo endelevu?  Juma hili tarehe 17 Oktoba ilikuwa siku ya kimataifa ya kutokomeza umasikini.

Maudhui ya mwaka huu yanalenga kuutizama umasikini kama sio tu kukosa kipato au chakula, ardhi na samani nyinginezo bali pia mambo mengine yachangiayo umasikini.

Ndiyo maana katika ujumbe wake kuhusu siku  hiyo,inayoadhimishwa kwa mara ya kwanza tangu kupitishwa ajenda 2030,  Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amesema ni muhimu kuheshimu ahadi za kujenga maisha ya amani, ustawi na utu kwa watu wote akiongeza kuwa inatupasa kutambua kwamba chuki na ubaguzi vinakwamisha jitihada za kuuondoa umasikini.

Makadirio ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa licha ya mafanikio makubwa tangu mwaka 2002 – idadi ya watu fukara inazidi kuongezeka ambapo mtu mmoja kati ya watu wanane bado anaishi katika umaskini uliokithiri, hii ikiwa ni pamoja na watu milioni 800 ambao hawana chakula cha kutosha.