Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yalaani vifo vya wakimbizi

UNRWA yalaani vifo vya wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA, limelaani shambulio lililowaua wakimbizi wanne wa Palestina wakati wa jaribio la kuondoka katika kambi ya wakimbizi iitwayo Khan Eshieh iliyoko Damascus nchini Syria.

Taarifa ya UNRWA ya kulaani mauaji hayo, imesema miongoni mwa waliokufa ni mwanaume mwenye umri wa miaka 60, na bintiye mwenye umri wa miaka 22, dereva wao na mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na mamaye, baada ya gari lao kupigwa kombora.

UNRWA imetaka kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa za kibinadamu, ili kulinda raia kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Ulinzi mkali katika eneo hilo umepunguza fursa ya raia kutoka eneo moja kwenda jingine kwa usalama na kupata misaada ya kibinadamu ikiwamo wa kiafya limesema shirika hilo.