Dawa ya Syria ni wahusika kutambua kuwa watawajibika- Pinheiro

21 Oktoba 2016

Huko Geneva, Uswisi hii leo Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limekuwa na kikao maalum kuhusu madhila yanayokumba wakazi wa Aleppo nchini Syria ambapo mwishoni wajumbe watapitisha azimio.

Akihutubia wajumbe , Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein amesema tena kuwa wajibu wa kumaliza mzozo wa Syria uko mikononi mwa Baraza la Usalama la Umoja.

Ametaka wajumbe kwenye hitimisho lao kusisitiza umuhimu wa kuwajibisha pande husika kwenye mzozo wa Syria ambao tangu uanze mwaka 2011 umesababisha vifo vya watu zaidi ya 300,000 na nusu ya wananchi wamekimbia makazi yao.

Naye mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Mataifa inayochunguza Syria, Paulo Pinheiro amesema..

(Sauti ya Pinheiro)

“Watekelezaji wa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu watakoma kukiuka sheria pindi wakifahamu kuwa watawajibishwa. Ndio maana hoja ya kuwasilisha suala la Syria ICC au mfumo unaoweza kuanzishwa kusaka haki, ni muhimu kutatua mgogoro huo.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter