Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi cha usalama Sudan Kusini kitaimarisha amani: Mogae

Kikosi cha usalama Sudan Kusini kitaimarisha amani: Mogae

Kupelekwa kwa kikosi cha ulinzi nchini Sudan Kusini ni hatua muhimu katika kusaka amani nchini humo amesema Mwenyekiti wa Kamisheni ya pamoja ya kufuatilia na kutathmini hali nchini humo JMEC, Festus Mogae.

Mogae ambaye ni Rais mstaafu wa Botswana ameyasema hayo wakati wa ufunguzi mkutano wa wadau katika mchakato wa amani ambapo amesema kuw ahakuna shaka kuwa hali mjiniJuba sasa ni shwari lakini utulivu huo waweza kuwa wa muda mfupi.

Kikosi cha askari karibu 4,000 kilidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Agosti mwaka huu kwa ajili ulinzi wa ziada kufuatia mapigano mapya yaliyoibuka mwezi Julai na kitakuwa chini ya ujumbe waUmoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS).

Mwenyekiti huo amesema kuwa kikosi hicho kinahitajika ili kuleta kuaminiana, usalama, kujenga amani na kuwezesha kuanza kwa utekelezaji wa umoja wa makubaliano.

Bwana Mogae ameomba kusitishwa mara moja kwa mapigano akitoa onyo kuwa kuendelea kwa uhasama kunaweza kusababisha vurugu zaidi.