Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pazia lafungwa, ajenda mpya ya miji yapitishwa sasa ni utekelezaji:Clos

Pazia lafungwa, ajenda mpya ya miji yapitishwa sasa ni utekelezaji:Clos

Mkutano mkubwa kabisa wa mustakhbali wa miji duniani kwa miaka 20 ijayo, umefunga pazia hii leo mjini Quito, kwa Katibu mkuu wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa tatu wa makazi HABITAT III kutangaza kuwa “historia imeandikwa kwa pamoja”

Joan Clos, ambaye pia ni mkurugenzi wa shirika la Umoja wa mataifa la makazi UN-HABITAT amesema mkutano huo ambao rasmi unajulikana kama mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya makazi na maendeleo endelevu mijini umekuwa wa mafanikio.

(SAUTI JOAN CLOS)

Mkutano umekuwa wa mafanikio kwa sababu umeandaliwa kwa muda mrefu na umekuwa na ushiriki mzuri, na umeturuhusu kufanya uchambuzi wa kina wa nini kilichoendelea katika miaka 20 iliyopita katika suala la ukuaji wa miji.”

image
Mtaa duni wa Mathare jijini Nairobi.(Picha:UM/ Julius Mwelu/ UN-Habitat
Mkutano huo umewaleta pamoja watu takribani 36,000 kutoka nchi 142 duniani katika siku sita zilizopita. Bwana Clos amesema ajenda mpya ya miji iliyopitishwa leo sasa kuingia kwenye azimio la Quito kuhusu miji na makazi endelevu kwa wote.ni lazima ichukuliwe kama nyongeza ya ajenda ya 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu iliyoafikiwa nan chi wanachama 193 mwezi Septemba mwaka 2015 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Malengo hayo 17 ya maendeleo au SDG’s yanatambua uwezo wa miji ambao utachukua karibu asilimi 70 ya watu wote duniani ifikapo 2050, kuwa ni kiungo cha ukuaji endelevu katika siku za usoni.

(SAUTI CLOS)

“Huu ndio mtazamo wa ajenda mpya ya miji na ninauhakika nchi wanachama watabaini nini kinachoendelea na pia kwa ushirikiano wa watu kwa sababu kwa pamoja tutawkuunda musthakbali bora mijini”

image
Mkutano wa makazi HABITAT III.(Picha:UM//Eskinder Debebe)
Ajenda hiyo amesema itazitaka nchi wanachama au serikali ya miji kuwa na malengo Fulani, lakini ameongeza kuwa ni mtazamo wa pamoja ambao umeweka viwango vya kubadilisha miji kuwa mahala salama, panapohimili mikiki na mahali endelevu kutokana na mipango bora na maendeleo.

Kwa kutia saini azimio hilo nchi waanchama wanajidhatiti kuchukua hatua katika miaka 20 ijayo kuboresha maeneo yote ya maisha ya mijini kupitia utekelezaji wa mpango wa Quito. Amesema utekelezaji ni lazima uanze mara moja

(SAUTI YA CLOS)

“Kama tusipotekeleza basi itakuwa kazi bure”