FAO na NEPAD kuinua ajira ya vijana Benin, Cameroon, Malawi na Niger

20 Oktoba 2016

Shirika la chakula na kilimo FAO na ushirika mpya kwa maendeleo ya Afrika NEPAD wamejumuisha nguvu ili kuongeza ajira na fursa za biashara kwa vijana wavijijini nchini Benin, Cameroon, Malawi na Niger.

Juhudi hizo zitawezeshwa na ufadhili wa dola milioni nne zilizotolewa na mfuko wa mshikamano kwa Afrika (ASTF).

Makubaliano yaliyotiwa saini Jumatano baina ya mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da SilvaAfisa mtendaji wa kitengo cha uratibu na mipango cha NEPAD kilijulikanacho kama NPCA, bwana Ibrahim Assane Mayaki, yatasaidia nchi hizo nne kuunda na kutekeleza sera ambazo zitainua maendeleo vijijini ikiwemo kuhamisha elimu na utaalamu.

Da Silva amesema ushirikiano huu unataka kuchagiza ajira zenye hadhi kwa vijana vijijini na ujasiriliamali katika sekta ya kilimo na biashara, na unawakilisha mfano mwingine muhimu unaoonmgozwa na Afrika katika kuhakikisha uhakika wa chakula na maisha bora katika bara hilo.

Kutimiza ajenda ya Afrika yam waka 2063 kutategemea kwa kiasi kikubwa mabadiliko vijijini yatakayowezesha wajasiliamali vijana katika mfumo wa chakula amesema bwana Mayaki.

Malengo ya mradi huu wa pamoja yanakwenda sanjari na azimio la mwaka 2014 la Malabo Declaration kupitia ahadi za Muungano wa Afrika za kutimiza malengo ya kilimo ifikapo 2025.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud