Afrika yaongoza kwa kuwa na miundombuni duni ya waenda kwa miguu

20 Oktoba 2016

Kenya, Malawi, Zambia na Afrika Kusini zimetajwa kuongoza katika nchi zilizo na miundombinu isiyo rafiki kwa waendesha baiskeli na waenda kwa miguu. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Taarifa hizo zimo kwenye ripoti iliyotolewa leo na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, ikiangazia maendeleo ya miundombinu kwenye nchi 20 za kipato cha chini na kati barani Afrika, Asia na Amerika ya kusini.

Ripoti imeeleza kuwa nchini Malawi pekee, asilimia 66 ya ajali za barabarani zilikumba waenda kwa miguu na waendesha baiskeli huku Kenya ikifuatia na asilimia 61.

UNEP imetaka uwekezaji zaidi kwenye miundombinu hiyo iwapo dunia inataka kupunguza hewa chafuzi itokanayo na matumizi ya magari.

Imependekeza serikali kutenga angalau asilimia 20 ya bajeti zao kwa ajili ya miundombinu ya waenda kwa miguu na waendesha baiskeli ili kuokoa maisha na kupunguza hewa ya ukaa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter