Mjadala umemalizika, kazi utekelezaji makubaliano DRC: Ban

Mjadala umemalizika, kazi utekelezaji makubaliano DRC: Ban

Mjadala wa kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC umemalizika, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon , amempongeza mwezeshaji wa Muungano wa Afrika katika majadiliano hayo Edem Kodjo, na washiriki wote, kwa kazi na juhudi zao za kuelekea suluhu ya amani katika mgogoro wa nchi hiyo hususani katika mchakato wa uchaguzi. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Kupitia taarifa ya msemaji wake, Ban amesema anatumai kwamba utekelezaji wa makubaliano utachangia mazingira bora yatakayoheshimu haki za msingi na uhuru ambao ni muhimu kwa mjadala wa kisiasa na uchaguzi.

Akizungumzia hitimisho la mjadala huo ulioshuhudia pia kutiwa saini makubaliano ya kisiasa, David Gressly, Naibu Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO amesema..

(Sauti ya David)

“Tunasihi pande zote DRC kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya maslahi yao binafsi au ya kichama na kuungana pamoja kwenye mchakato huu ili hatimaye kuweka fursa ya mashauriano ya sauti moja na kumaliza kwa amani mkwamo wa mchakato wa uchaguzi.”