Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maagano ya haki za binadamu yatafanikisha SDGs- Eliasson

Maagano ya haki za binadamu yatafanikisha SDGs- Eliasson

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema ajenda ya maendeleo endelevu, SDGs inatoa fursa ya kutekeleza kwa dhati maagano mawili ya haki za binadamu yaliyopitishwa nusu karne iliyopita.

Amesema hayo leo akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya maagano hayo ambayo ni azimio la haki za binadamu na agano kuhusu haki za kiraia na kisiasa lililofuatiwa na itifaki ya kiuchumi na kijamii.

Eliasson amesema katika dunia ambayo imejaa vita, machungu, umaskini na ubaguzi, miaka 50 ya maagano hayo ni fursa sahihi ya kushikamana na misingi na dira yao.

Amesema kwa mantiki hiyo kwa kuzingatia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo za kisiasa, kiraia, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, maagano hayo ni muhimu zaidi sasa na yatachagiza ajenda 2030 na uwajibikaji.