Mapigano yasiyokwisha CAR yasababisha njaa:WFP

19 Oktoba 2016

Mapigano ya hivi karibuni katika eneo la Kaga Bandoro nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) yamelilazimu Shirika la mpango wa Chakula Duniani, WFP kupeleka haraka msaada wa chakula kwa watu 8,000 walioathirika zaidi.

WFP inasema operesheni hiyo ya dharura iliyoanza tarehe 17 Oktoba tayari imesambaza mgao wa siku 15 kwa watu 5,000, waliokimbia na kusaka hifadhi nje ya jengo la Umoja wa Mataifa katika mji wa Kaga Bandoro, na wengine 3,000 katika mji wa Ganama.

Shirika hilo pia limesema linawasiwasi mkubwa na mapigano yasiyokwisha CAR, na lina mpango wa kusaidia watu milioni 1.4, ingawa hadi sasa ombi la kuendesha shughuli hizo limefadhiliwa kwa asilimia 44 tu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter